APPLY NOW

WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR

 

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI. 

Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa chini ya  Sheria Namba 2/2006 na Marekebisho yake Namba 3/2017.

Lengo kuu la kuanzishwa Taasisi hii ni kusimamia Udhibiti wa Ubora na Usalama na wa Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa vya Utibabu, ili kulinda Afya za Jamii ya Zanzibar.

Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) inakaribisha maombi kwa ajili ya kujaza nafasi katika Ofisi yake ya Pemba kwa waombaji wenye sifa stahiki.

Nafasi yenyewe ni:-

v  MKURUGENZI OFISI YA PEMBA.

Sifa za muombaji:

      i.        Awe Mzanzibari;

     ii.        Awe na elimu isiyopungua shahada ya kwanza katika fani ya Famasia au inayolingana.

    iii.        Awe na uwezo wa kufanya kazi bila ya kusimamiwa.

    iv.        Awe na uwezo wa kusimamia na kuongoza.

     v.        Awe na uzoefu wa kazi katika fani husika usipongua miaka mitano.

    vi.        Mwenye taaluma zaidi katika Fani husika atapewa kipaumbele.

   vii.        Mshahara ni kwa mujibu wa ngazi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 viii.        Awe tayari kufanya kazi katika muda wa ziada/dharura. 

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI.

Muombaji anatakiwa aandike barua ya maombi na kuambatanisha na vitu vifuatavyo:

a)    Maelezo binafsi ya muombaji (CV).

b)    Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo.

c)    Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.

d)    Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.

e)    Picha moja ya muombaji (Passport size) iliyopigwa karibuni.

f)     Majina na Anuani za Wadhamini wawili wanaotambulika.

g)    Anuani rasmi anayopatikana muombaji, barua pepe na nambari ya simu.

MAMBO YA KUZINGATIWA

       i        Muombaji atakaewasilisha “Statement of Result” au Progressive Report” maombi yake hayatazingatiwa.

     ii        Muombaji wa Serikali maombi yake yapitie kwa muajiri wake vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

    iii        Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na ziwasilishwe moja kwa moja Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar iliyopo maeneo ya Mombasa barabara ya Changu kuelekea Tomondo wakati wa saa za kazi.

    iv        Siku ya mwisho kupokea maombi ni Ijumaa Tarehe 29/05/2020 saa 9:30 Alaasiri.

      v        Mawasiliano yatafanywa kwa wale watakaopita katika mchujo wa awali (short list).

 

Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

 

MKURUGENZI MTENDAJI,

WAKALA WA CHAKULA NA DAWA,

S.L.P 3595,

ZANZIBAR.

Days
Hours
Minutes
Seconds
29/05/2020: 03:30 PM TUNAOMBA RADHI KUA MUDA WA KULETA MAOMBI UMESHAPITA. TUNATOA SHUKRANI KWA WALE WOTE WALIO OMBA NAFASI HII. "TUNAKUTAKIENI KILA LA KHERI"
Share on facebook
Facebook
Share on twitter
Twitter
Share on whatsapp
WhatsApp