You are currently viewing TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

  • Post author:
  • Post category:ZFDA

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya inayofanyakazi kwa mujibu wa Sheria nambari 2 ya Mwaka 2006 ambayo ilifanyiwa marekebisho kupitia Sheria nambari 3 ya Mwaka 2017.

ZFDA ni Taasisi iliyoanzishwa kwa lengo la kulinda na kuimarisha afya ya umma kupitia udhibiti wa usalama wa ubora wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na bidhaa nyingine zinazohusiana na afya kwa kufanya usajili, ukaguzi, uchunguzi wa kimaabara na udhibiti wa uingizaji na utoaji wa bidhaa hizo nchini.

ZFDA katika kuimarisha utendaji wa kazi na kufikia malengo ya kuanzishwa kwake inakaribisha maombi ya ya kujaza nafasi ya Mkurugenzi wa ndani katika Ofisi yake ya Pemba kwa waombaji wenye sifa stahiki.

Nafasi yenyewe ni:

  1. MKURUGENZI OFISI YA ZFDA – PEMBA (Daraja ZPS-EX-38)

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Famasia (Pharmacy) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uzoefu wa kusimamia masuala ya udhibiti (Regulatory Affairs)
  • Awe na uzowefu wa kazi usiopungua miaka 7.
  • Kusoma, Kuandika na kuongea lugha ya Kingereza ni sifa ya ziada.

 

 

Majukumu:

  1. Kusimamia ukaguzi wa bidhaa, majengo na shughuli zinazohusiana na bidhaa zinazodhibitiwa kwa upande wa Pemba;
  2. Kudhibiti usafirishaji ndani na nje ya kisiwa cha Pemba kwa bidhaa zinazodhibitiwa;
  • Kusajili na kutoa vibali vya majengo ya bidhaa zinazodhibitiwa;
  1. Kufanya ufuatiliaji wa bidhaa zilizopo katika mzunguko wa soko (PMS) na shughuli za uangalizi wa dawa na vifaa vya tiba;
  2. Kusimamia majengo ya ofisi na vituo vya kutoa huduma;
  3. Kusimamia rasilimali za taasisi ikiwemo rasilimali watu, fedha, na vitendea kazi;
  • Kuongeza uelewa kuhusu huduma za taasisi kwa wadau na umma kwa ujumla;
  • Kukuza ushirikiano na uratibu na mamlaka za serikali za mitaa na wadau wengine;
  1. Kuratibu na kufanya tafiti, programu na miradi inayohusiana na huduma za taasisi;
  2. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.

 

JINSI YA KUOMBA:

 

  • Muombaji anatakiwa kuwasilisha maombi yake moja kwa moja katika ofisi ya ZFDA – Unguja.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo: –

 

  1. CV ya Muombaji.
  2. Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo na kwa wale waliosoma nje ya nchi, wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya uthibitisho kutoka TCU.
  3. Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
  4. Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
  5. Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
  6. B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
  7. Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 07/01/2026, saa 9:30 Alaasiri.
  8. Barua zote za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

 

 

MKURUGENZI MTENDAJI,
WAKALA WA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR

S.L.P 3595 – ZANZIBAR.

 

Tangazo hili linapatikana pia katika Tovuti ya Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) ambayo ni www.zfda.go.tz


Download