ZANZIBAR FOOD AND DRUG AGENCY

Together We Protect Public Health

Elimu kwa umma juu ya Usalama wa Chakula na Madhara yatokanayo na Dawa, yalitolewa kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikindani, Dole , 21/09/2023

Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), imetoa elimu kwa wanafunzi wa Sekondari wa Skuli ya Mikindani iliyopo Dole, mnamo tarehe 21/09/2023.

Wanafunzi hao walipatiwa elimu juu ya Usalama wa Chakula, Madhara yatokanayo na Dawa na namna ya kuripoti madhara hayo.

Aidha, wanafunzi walipata fursa ya kuona Vipodozi mbali mbali ambavyo vina viambata sumu (Vipodozi Haramu), na hivyo kushauriwa kutonunua au kutumia vipodozi hivo au vyovyote vile ambavyo vina viambata sumu.

ZFDA inaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kujenga uelewa juu ya usalama wa Chakula, Dawa na Vipodozi ili kuhakikisha afya za wananchi zinabaki kuwa salama.

"Together we protect public health"