You are currently viewing TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

 

 

JUU YA CLIP INAYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU BIDHAA ZA NAFAKA ZILIZOCHANGANYWA NA CHAKULA CHA MIFUGO/NGURUWE

Wakala wa Chakula na Dawa (ZFDA) inapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa kuna Clips zinazoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii (WhatsApp) ambazo zinamuonesha Afisa alievalia T-Shirt yenye nembo ya CRDB akipekua bidhaa za nafaka (mchele na maharagwe) ambazo kwa muonekano wa juu zinaonekana zikiwa zinavutia kwa wanunuzi. Lakini anapojaribu kuingiza mkono chini ya nafaka hizo na kupekua kwenye magunia inaonekana mchele ukiwa umefanya madonge madonge na mwengine kuwa mweusi sana na maharagwe kuchanganywa na taka kata nyengine pamoja na vumbi jingi.

 

ZFDA inapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa bidhaa ambazo zinaonekana katika Clips hizo hazipo katika soko la Zanzibar. ZFDA inapenda kuwashauri wananchi wote kuendelea kuwa waangalifu pindi wanapofanya ununuzi wa bidhaa mbali mbali kwa matumizi yao kuhakikisha zinakua bora na salama.

 

Vile vile, ZFDA inapenda kutumia fursa hii kuwakumbusha wananchi kuendelea kutoa taarifa pale wanapoona bidhaa ambazo wanazishukia kuwa hazipo salama kuwepo katika maeneo ya masoko, maduka na ghala au sehemu yoyote ile kwa ajili ya kuchukua hatua zinazofaa kabla ya kuleta athari kwa watumiaji.

 

 

imetolewa na kitengo cha uhusiano na masoko zfda

Please follow and like us: