ZANZIBAR FOOD AND DRUG AGENCY

Together We Protect Public Health

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU DAWA YA CARBOTOUX

UWEPO WA TAARIFA INAYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU DAWA YA CARBOTOUX YENYE KUSABABISHA MADHARA KWA MTUMIAJI Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu video inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuanzia tarehe 26/11/2023, ikimuonesha mtu anaetapika damu huku ikihusishwa na utuamiaji wa Dawa aina ya CARBOCISTEINE-PROMETHAZINE SYRUP yenye jina […]

TANGAZO LA MAFUNZO YA KIVITENDO

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi, inawatangazia wadau wote kwamba, maombi ya usajili wa Mafunzo ya Kivitendeo ya Wafamasia Watarajali (Internship) kwa muhula unaoanza Januari 2024 yameanza kupokelewa rasmi kuanzia mwezi Novemba 2023 hadi tarehe 25 Disemba 2023.

CUSTOMER SERVICE WEEK

ZFDA yaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kujumuika pamoja na wateja na kuwapatia vyeti vya shukrani. “Together We Protect Public Health”

UTEKETEZAJI WA BIDHAA ZA DAWA

Wakala wa Chakula na Dawa (ZFDA), imeteketeza jumla ya Tani 15 za bidhaa za Dawa zilizomaliza muda wake wa matumizi pamoja zile zilizoingia nchini kinyume na Sheria ya Wakala wa Chakula na Dawa. Zoezi hilo, limefanyika Kikungwi, Mkoa wa Kusini Unguka leo tarehe 23/09/2023. “Together we protect public health”

ELIMU KWA UMMA

Elimu kwa umma juu ya Usalama wa Chakula na Madhara yatokanayo na Dawa, yalitolewa kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikindani, Dole , 21/09/2023 Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), imetoa elimu kwa wanafunzi wa Sekondari wa Skuli ya Mikindani iliyopo Dole, mnamo tarehe 21/09/2023. Wanafunzi hao walipatiwa elimu juu ya Usalama wa Chakula, Madhara yatokanayo […]

WORLD FOOD SAFETY DAY

ZFDA Ikiadhimisha siku ya Usalama wa Chakula Duniani kwa Matembezi yaliyoanza Afisi za Mombasa na kumalizia Kisonge (Mapinduzi Square), Mgeni Rasmi wa Shughuli hio ni Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Maisha Bora Foundation Mheshmiwa Mama Mariam Mwinyi  10/10