You are currently viewing UFAFANUZI JUU YA TAARIFA INAYOSAMBAA KUHUSU TENDE INAYOMALIZIA MUDA WA MATUMIZI WA APRIL 2022

UFAFANUZI JUU YA TAARIFA INAYOSAMBAA KUHUSU TENDE INAYOMALIZIA MUDA WA MATUMIZI WA APRIL 2022

  • Post author:
  • Post category:ZFDA

Wakala wa Chakula na Dawa (ZFDA) inapenda kuwaarifu wananchi wote kuwa kuna taarifa zinazoendelea kutumwa katika mitandao ya kijamii (WhatsApp) juu ya uwepo wa tende aina ya Majdool ya Kampuni ya AL SAIF DATES kutoka nchini Saudi Arabia ambayo inadhaniwa kuwa imepitwa na muda wake wa matumizi. ZFDA inapenda kuwatoa hofu watumiaji wote wa bidhaa hiyo kuwa bado inaendelea kuwa ni salama kwa matumizi ya binadamu hadi mwishoni mwa mwezi wa Aprili itakapokuwa imemaliza muda wake wa mwisho wa matumizi.

ZFDA inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa bidhaa ambazo zimeandikwa mwezi badala ya tarehe ya mwisho wa matumizi ni kwamba bidhaa hizo zinaendelea kutumika hadi mwishoni mwa mwezi husika uliotajwa wa mwisho wa matumizi badala ya mwanzoni mwa mwezi husika.

ZFDA inapenda kuwashauri wananchi wote kuendelea kuwa waangalifu wakati wa ununuzi wa bidhaa zao za matumizi kuhakikisha wanaangalia vizuri tarehe za ukomo wa matumizi yake, ubora wake na usalama wake kabla ya kuamua kununua bidhaa hizo na pia kuhakikisha wanadai risiti za manunuzi ya bidhaa hizo ili kurahisisha ufuatiliaji wake iwapo bidhaa hizo zitakuwa hazikukidhi vigezo husika. Vile vile ZFDA inapenda kutumia fursa hii kuwakumbusha wananchi kuendelea kutoa taarifa pale wanapoona bidhaa ambazo hazikidhi viwango kuwepo katika maeneo ya masoko, maduka na ghala au sehemu yoyote ile kwa ajili ya kuchukua hatua zinazofaa kabla ya kuleta athari kwa watumiaji.

Please follow and like us: