Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) inapenda kuwatangazia wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla kuwa wale wote wanaotaka kuchinja wanyama kwa kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Eid – el – Adh-ha wachinje wanyama hao katika machinjio yanayotambuliwa na ZFDA kwa mujibu wa kanuni ya nyama ya mwaka – 2015. Machinjio yafuatayo yatatumika kwa kipindi hiki cha Sikukuu.
KWA UNGUJA: Kisakasaka, Mwera, Muwanda, Kianga, Kinyasini, Mahonda na Mfenesini.
KWA PEMBA: Wete, Mkoani, Micheweni, Chake, Meli tano, Konde na Ole Kianga.
Kwa wananchi wote ambao wamepanga kuchinja nje ya maeneo yaliyotajwa kwa ajili ya Sikukuu ya Eid, wanaombwa kuwasilisha maombi yao katika ofisi za ZFDA ili kuweza kupewa taratibu wanazotakiwa kuzifuata.
Kwa maelezo zaidi fika katika ofisi zetu zilizopo Mombasa – Unguja na Wete – Pemba au wasiliana nasi kwa nambari za simu – 0718588584 /0777139968
ZFDA inawatakia kheri na matayarisho mema ya Eid- El Adh-ha