Wakala wa Chakula na Dawa (ZFDA) kwa kushirikiana na Manispaa za Mkoa wa Mjini Magharibi zinapenda kuwatangazia wafanyabiashara wote kuwa, ifikapo tarehe 20/07/2020, kwa mujibu wa Sheria namba 2 ya 2006 ya Chakula, Dawa na Vipodozi itakuwa ni marufuku kupanga bidhaa za vipodozi na chakula kama vile sabuni za kuogea, Mafuta ya kujipaka, losheni, krimu, mchele, chumvi, soda, maji, mafuta ya kula n.k nje ya maduka.
Yeyote atakaekwenda kinyume na tangazo hili hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Kwa maelezo zaidi wafanyabiashara wanatakiwa kufika katika afisi za ZFDA zilizopo Mombasa Barabara ya Changu na Manispaa husika wakati wa saa za kazi.