You are currently viewing TANGAZO

TANGAZO

  • Post author:
  • Post category:Public / ZFDA

Wakala wa Chakula na Dawa (ZFDA) inawatangazia wafanyabiashara wote wa maziwa kuwa, ifikapo tarehe 20 Februari 2020, kwa mujibu wa Sheria namba 2 ya 2006 ya Chakula, Dawa na Vipodozi na Kanuni ya maziwa ya mwaka 2011 itakuwa ni marufuku:-

  1. Kuuza maziwa katika maeneo ya wazi, kama vile maeneo ya  nje ya masoko na pembezoni mwa barabara.

2. Kusafirisha na kuuza maziwa katika vyombo vya plastiki kama vile chupa za plastiki na madumu.

Yeyote atakaekwenda kinyume na tangazo hili hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Kwa maelezo zaidi wafanyabiashara wanatakiwa kufika katika afisi za ZFDA zilizopo Mombasa Barabara ya Changu kwa Unguja na Afisi za ZFDA Wete kwa Pemba wakati wa saa za kazi.

Tangazo hili limetolewa na

MKURUGENZI MTENDAJI

WAKALA WA CHAKULA NA DAWA

Simu: 0242233959 au 0777139968

Please follow and like us: