You are currently viewing ZFDA WAPIGA MARUFUKU CHOKLET NA JUISI FRUT ZILIZOMO KWENYE VIFUNGASHIO VYA BOMBA LA SHINDANO

ZFDA WAPIGA MARUFUKU CHOKLET NA JUISI FRUT ZILIZOMO KWENYE VIFUNGASHIO VYA BOMBA LA SHINDANO

Wazazi na Walenzi nchini wametakiwa kuepuka kuwanunulia Watoto wao bidhaa aina ya Choklet zilizotengenezwa mfano wa Bomba ya Sindano kutokana na kuingizwa nchi kimagendo bila kuthibitishwa ubora na usala wake kwa watumiaji.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Usalama wa Chakula (ZFDA) Dr. Khamis Ali Omar wakati akizungumza na Wanahabari Ofisini kwake Mombasa mjini Zanzibar kuhusu uwepo wa bidhaa hiyo katika Soko.

Amesema Muingizaji wa Bidhaa hizo hakupita katika Ofisi yake hivyo bidhaa hizo bado hajizasajiliwa wala kupita katika Maabara yao kujulikana ubora na usalama wake.

Aidha Dk. Khamis ameongeza kuwa ZFDA kwa kushirkiana na vyombo vingine vya uchunguzi wanaendelea kumtafuta Mfanyabishara aliyeziingiza bidhaa hizo nchini kinyume na sheria na akipatikana atapelekwa katika vyombo vya Sheria. “Jukumu la ZFDA kwa sasa ni kuziondoa katika Soko kutokana na kutokidhi vigezo wakati huo huo kwa kushirikiana na vyombo vingine tunamtafuta Mfanyabiashara huyo ili tumpeleke katika vyombo vya kisheria”

Kwa upande wake mkuu wa Kitengo cha usajili wa bidhaa kutoka ZFDA Khadija Ali Sheha amesema bidhaa hiyo siyo halisi kwa vile haioneshi hata Kampuni au Kiwanda kilichotumika kutengeneza bidhaa hiyo.

Amesema katika Vifungashio vya Bidhaa hiyo imeandikwa inatoka nchini China lakini hakuna maelezo ya ziada kuelezea Kiwanda kilichotumika na Jimbo husika nchini China ili kufuatilia zaidi.

Kuhusu kifungashio chake amesema bidhaa hiyo inamlaghai mtoto na hivyo zinaweza kupelekea athari kubwa kwa watoto siku za mbele. “Kifungashio kinamlaghai mtoto lakini kinaweza pia kuwapelekea Watoto waweze hata kutumia Mabomba ya Sindano ya kawaida kutia maji au juisi wakaanza kutumia na mwisho kupata maambukizi mbalimbali” Alisema Khadija.

Kutokana na hali hiyo tayari Wakala unaendelea na zoezi la kuzichuguza bidhaa hizo katika maeneo tofauti ili zisiwepo katika Soko.

Mohamed Shadhil Shauri Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula ZFDA amesema tayari wamekagua @ Zanzibar Food and Drug Agency – ZFDA

Please follow and like us:

This Post Has 2,403 Comments