KUYAONDOA SOKONI MAJI YA NUSU LITA (500 ML) YA “LOOTAH GROUP OF COMPANY”

KUYAONDOA SOKONI MAJI YA NUSU LITA (500 ML) YA “LOOTAH GROUP OF COMPANY”

KUYAONDOA SOKONI MAJI YA NUSU LITA (500 ML) YA “LOOTAH GROUP OF COMPANY” KUTOKANA NA MATATIZO YA KITAALAM (RECALLS OF DRINKING WATER FROM “LOOTAH GROUP OF COMPANY” DUE TO TECHNICAL PROBLEM)

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya – Zanzibar inayosimamia udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa na vipodozi. Miongoni mwa kazi zake ni kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zilizotajwa aidha ziwe zinazalishwa hapa nchini au zinazoingia nchini ni salama kabla kumfikia mtumiaji. Hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali juu ya uwepo wa maji ya kunywa kutoka katika Kampuni ya “Drop of Zanzibar” yenye ujazo wa nusu lita (500 ml). Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar imefanya ukaguzi katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar na kujiridhisha kuwa maji hayo yana matatizo ya kitaalam katika utengengenezwaji wake.
Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar inapenda kuwapa taarifa wauzaji na watumiaji wa maji hayo kuwa maji yenye ujazo wa nusu lita kutoka Kampuni ya “LOOTAH GROUP OF COMPANY” ambayo yamezalishwa kuanzia tarehe 01/04/217 hadi 30/06/2017 yana tatizo la kitaalamu na hivyo basi hayaruhusiwi kusambazwa, kuuzwa na kutumika kwa matumizi ya binadamu.
Hivyo basi Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar inapenda kuchukua fursa hii kuwajulisha wale wote ambao wana bidhaa hiyo ambayo imetengenezwa katika muda huo uliotwaja kuacha kuziuza mara moja na kutoa taarifa kwa Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar na kuzirudisha kwa Kampuni ya “LOOTAH GROUP OF COMPANY” kwa ajili ya hatua zinazofaa za kuchukua ikiwemo kurejesha maji hayo katika Kampuni hiyo.
Vile vile, Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar inapenda kuchukua fursa hii kuwajulisha Kampuni ya “LOOTAH GROUP OF COMPANY” kuhakikisha kuwa bidhaa hiyo wanaiondoa sokoni si zaidi ya wiki moja kuanzia tarehe 25 Agosti hadi tarehe 01 Septemba 2017.
Kwa maelezo zaidi tafadhali fika katika ofisi za ZFDA Mombasa (mkabala na soko la mboga mboga)- Zanzibar Au piga simu namba 0777 139 968 nyakati za saa za kazi.

Imetolewa na
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji
ZFDA
25 Agosti 2017